Mazingira FM

Changamoto ya Maji, walimu, maktaba na uzio wa Shule bado ni tatizo shule ya Sekondari Bunda Day

28 October 2022, 4:43 pm

Changamoto ya uzio, maktaba, upungufuwa walimu wa sayansi na maji bado ni changamoto inayoikabili shule ya Sekondari Bunda day iliyoko kata ya kabarimu Halmashauri ya Mji wa Bunda mkoani Mara.

Hayo yamebainishwa katika maafali ya wahitimu wa kidato Cha Nne 2022 Bunda Day kupitia risala ya wahitimu na taarifa ya shule kupitia kwa Mkuu wa Shule hiyo.

Katika risala ya wahitimu wamesema changamoto kubwa inayoikabili shule hiyo ni maktaba ambapo inachangia wanafunzi kutokupata sehemu nzuri ya kujisomea pia suala la Maji ya kutumia


Kwa upande wake mkuu wa Shule ya Sekondari Bunda Day Charles Somba Amesema pamoja na maji kuwa na changamoto katika shule hiyo Ila ukosefu wa uzio na upungufu wa walimu bado ni tatizo

Kwa upande wake mgeni rasmi katika maafali ya shule hiyo Muhunda Manyonyoryo ambaye pia ni Diwani wa kata ya kabarimu amesema zile changamoto zilizoainishwa katika risala na taarifa ya shule atazifikisha katika mamlaka husika ili ziweze kutatuliwa

Aidha Mhe Muhunda ametoa kilo 70 za Mchele kuwasaidia wanafunzi wa hao kama chakula kipindi Cha mitihani wa kidato Cha Nne unaotarajiwa kuanza kufanyika tarehe 14 Nov 2022