Mazingira FM

Wakazi wa Mcharo Sasa waanza kunywa maji ya Bomba

27 September 2023, 12:45 pm

Meneja RUWASA akiwa na wakazi wa Mcharo akifungulia koki ya maji kudhihirisha upatikana wa huduma ya maji bombani kuanza.Picha na Adelinus Banenwa

Wakazi wa Mcharo Sasa waanza kunywa maji ya Bomba ni ule mradi unaotekelezwa na RUWASA ambao mwenyekiti wa mtaa alinusurika kupigwa

Na Adelinus Banenwa

Wakazi wa Mcharo Sasa waanza kunywa maji ya Bomba ni ule mradi unaotekelezwa na RUWASA ambao mwenyekiti wa mtaa alinusurika kupigwa kutokana na adha waliyokuwa wakiipata wananchi wa mtaa wa Mcharo na maeneo jirani.

Meneja RUWASA Eng William Boniphas aliahidi kutatua changamoto hiyo haraka chini ya wiki Moja wananchi watakuwa wamepata Maji

Wakazi wa Mcharo katika mkutano wakiomba ufafanuzi wa baadhi ya mambo kutoka RUWASA

Redio Mazingira Fm ilifika Mcharo siku ya jumapili kujua je maji yametoka ambapo ilizungumza na mwenyekiti wa mtaa ambaye alikiri maji hatajatoka isipokuwa mafundi wapo site wanaendelea na marekebisho madogo madogo, ikiwa ni pamoja na kuwekwa Kwa tank la lita 5000 Kwa wananchi wanaozunguka chanzo Cha maji, kusukuma Maji kwenda tenki kuu tayari Kwa kusambazwa miongoni mwa marekebisho mengine.

Charles Bupumula mwenyekiti wa mtaa wa Mcharo alisisitiza wakazi wa Mcharo wanataka maji.

Meneja wa RUWASA Eng William Boniphas alisema kufikia jumapili jioni Kila kitu kitakuwa kimekamilika na jukumu linalobaki ni Kwa upande wa mtaa kuchagua watu watakaosimama kwenye hivyo vituo vya maji ( DP ) kukusanya fedha akibainisha ndoo Moja ya lita 20 itauzwa shilingi 40 Kwa mujibu wa sheria

Eng William aliahidi kufanya kikao na wakazi wa Mcharo siku ya jumanne chenye lengo la kuwajulisha kwamba maji yanatoka pili utaratibu uliopo katika kutumia hayo maji ili itokee upotevu wa Maji

Update ya jumanne.

Pichani ni Meneja RUWASA Eng William Boniphas akifungulia koki ya maji katika moja ya DP kuashiria huduma imeanza kupatikana. Picha na Adelinus Banenwa

Siku ya jumanne Mazingira Fm ilifika tena Mcharo ili kufahamu kwanza maji yanatoka na nini maazimio ya RUWASA na wakazi wa Mcharo katika mradi huo

Radio Mazingira ilishuhudia wananchi wakifurahia huduma ya maji baada ya wataalamu kutoka RUWASA Wakiongozwa na na Meneja kufungu maji na kuanza kutoka bombani

Wananchi hawakuacha kuipongeza redio Mazingira Kwa kusaidia kupaza sauti hadi sasa maji yametoka

Aidha walimuomba Meneja RUWASA kurekebisha vituo vingine ambavyo vilikuwa havitoi maji viweze kutoa Kwa kuwa kati ya vituo na ni vinne tu vilivyotoa maji huku vingine vinne havikutoa.

Akijibu ombi Hilo Meneja wa RUWASA amesema mradi haujakamilika amewaachia fundi wa mamlaka hiyo ili kutatua changamoto hizo ndogondogo huku akiwataka wakazi wa Mcharo kulinda miundombinu hiyo na kutojihusisha nahujuma za aina yoyote.