Mazingira FM

Sekondari Kabasa yapigwa jeki

6 October 2023, 8:39 am

Kambarage Wasira, mgeni rasmi mahafali kidato cha 4 mwaka 2023 Kabasa Sekondari

Mahafali ya kidato cha nne shule ya sekondari Kabasa, Kambarage Wasira akiwa mgeni rasmi atoa milioni moja (1,000,000/=Tsh) kukabili sehemu ya changamoto katika shule hiyo.

Na Edward Lucas

Ikiwa ni wiki moja imepita tangu Kambarage ashiriki mahafali ya darasa la saba shule ya msingi Kunzugu na kutoa ahadi ya mashine ya kuchapisha ‘printer’ yenye thamani ya shilingi milioni moja na laki 2 (1,200,000/=) hii leo ilikuwa ni zamu ya sekondari Kabasa akiwa mgeni rasmi tena.

Katika mahafali hayo, Kambarage Wasira ametoa shilingi milioni 1 ili kusaidia sehemu ya changamoto zinazoikabili shule hiyo.

Sauti ya Kambarage Wasira
Godfrey Maige Maduhu, Mkuu wa shule ya Sekondari Kabasa. Picha na Edward Lucas

Awali akisoma taarifa ya shule, mkuu wa shule hiyo, Godfrey Maige Maduhu amebainisha changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo kuwa ni pamoja na ukosefu wa bwalo, maktaba, upungufu wa walimu na upungufu wa matundu ya choo 24 huku akiipongeza serikali ya awamu ya sita kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa kwani shule hiyo ina madarasa ya ziada 6.

Sauti ya Godfrey Maige Maduhu
Grace Raymond akisoma risala ya wahitimu kidato cha 4 Sekondari Kabasa ikibainisha baadhi ya changamoto walizokumbana nazo
Sauti ya Grace Raymond