Mazingira FM
Mazingira FM
20 May 2026, 2:01 pm

Watu walio na uhitaji wa hali ya juu zaidi wa damu ni pamoja na manusura wa ajali, akina mama wanaojifungua watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
Na Adelinus Banenwa
Wito umetolewa kwa wananchi kujenga utamaduni wa kuchangia damu kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili kutimiza kauli mbiu ya mpango huo wa ” changia Damu okoa maisha”
Akizungumza kupitia kipindi cha Asubuhi leo kinachorushwa kupitia Radio Mazingira fm Stephano Machage mratibu wa mpango wa damu salama kutoka halmashauri ya mji wa Bunda amesema kuna faida nyingi mwananchi anapojitolea kuchangia damu kwa hiari badala ya kuchangia pindi unapokuwa na mgonjwa.
Amesema zamani ilikuwa ni ngumu sana kuokoa maisha ya wananchi wanohitaji damu kutokana na utaratibu uliyokuwepo kwamba mgonjwa akiitaji damu basi ndugu wanakusanywa kisha anapimwa mwenye group kama lake ndipo atolewe damu na kuwekewa mgonjwa hali iliyokuwa inapelekea wagonjwa kuwa kwenye hatari ya kupoteza maisha.
Machage ameongeza kuwa tangu mpango wa kuwa na benki ya damu salama uanze umekuwa jibu sahihi katika kuokoa maisha ya wagonjwa kwa wakati kutokana wananchi hujitolea damu kwa hiari na wataalamu hufanya vipimo ili iwe damu salama.
Machage amesema watu walio na uhitaji wa hali ya juu zaidi wa damu ni pamoja na manusura wa ajali, akina mama wanaojifungua watoto wenye umri chini ya miaka mitano ambapo mbani kutoa elimu hiyo amehamasisha wananchi kuchangia damu kutokana na mpango uliopo kwa wachangia damu kwa hiari hutambuliwa na mamlaka kwa kumpatia kadi inayoweza kumsaidia baadaye