Mazingira FM

UWT Bunda watembelea wagonjwa hospitali ya Manyamanyama

23 October 2023, 9:18 am

Wajumbe wa Baraza la UWT wakiwa katika hospitali ya Manyamanyama kuonesha matendo ya huruma kwa wagonjwa.

UWT Bunda watembelea hospitali ya Manyamanyama-Bunda kuonesha matendo ya huruma kwa wagonjwa katika kuadhimisha kilele cha wiki ya UWT

Na Edward Lucas

Maadhimisho ya wiki ya Wanawake UWT Wilaya ya Bunda mkoa wa Mara yamefikia kilele hapo jana 22 Oct 2023 kwa wajumbe kufanya matendo ya huruma kwa kutembelea wagonjwa hospitali ya Manyamanyama.

Wakiwa hospitalini hapo wajumbe hao wa UWT wakiongozana na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji CCM mkoa wa Mara ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Latifa Hamis walitembelea wodi ya wanawake na watoto wakiwajulia hali na kuwapa mahitaji mbalimbali kama sabuni na juisi.

Awali akitoa taarifa ya ujuio wa wajumbe hao kwa uongozi wa hospitali ya Manyamanyama Katibu UWT Bunda, Evodia Zumba alieleza kusudio la kufika hospitalini hapo.

Sauti ya Evodia Zumba, Katibu UWT Bunda

Naye Diwani wa Kata ya Manyamanyama, Mhe.Mathayo Machiru amewashukuru wajumbe hao kufika hospitali hapo kuonesha matendo ya huruma na kuushuru uongozi wa hospitali kuwapa fursa hiyo

Mhe. Mathayo Machiru, Diwani Kata ya Manyamanyama akitoa neno la shukurani kwa wajumbe UWT Bunda.Picha na Edward Lucas
Sauti ya Mhe. Mathayo Machiru

Wajumbe hao ambao ni wenyeviti na makatibu waliotoka Kata 33 za Wilaya ya Bunda walitembelea pia mradi wa ujenzi wa nyumba ya katibu wa UWT eneo la Manyamanyama kujionea utekelezaji wa ujenzi huo.

Wajumbe wa Baraza la UWT Wilaya ya Bunda wakiwa jengo la Katibu UWT linalojengwa eneo la Manyamanyama. Picha na Edward Lucas