Mazingira FM

Kambarage atatua changamoto ya maji Kunzugu sekondari

13 October 2023, 7:22 am

Ndugu Kambarage Wasira, Mgeni Rasmi maafali ya 16 shule ya Sekondari Kunzugu. Picha na Adelinus Banenwa

Kiasi cha shilingi million moja  laki moja na elfu Arobaini na nne (1,144,000) zimetolewa na Ndugu Kambarage Wasira katika kutatua changamoto ya maji shule ya sekondari kunzugu leo kwenye mahafali ya kidato cha nne.

Na Adelinus Banenwa

Kiasi cha shilingi million moja  laki moja na elfu Arobaini na nne (1,144,000) zimetolewa na Ndugu Kambarage Wasira katika kutatua changamoto ya maji shule ya sekondari kunzugu leo kwenye mahafali ya kidato cha nne.

Akijibu risala na taarifa ya shule ndugu Kambarage amesema pamoja na changamoto mbalimbali zilizoainishwa kupitia taarifa ya shule na risala ya wanafunzi amebaini suala la maji ni muhimu kwa ajili ya walimu na wanafunzi hasa ukizingatia maji hayana mbadala

Aidha amesema  kupitia upimaji wa mamlaka ya maji Bunda BUWSSA walianiasha ili maji yaweze kufika shuleni hapo ghalama ni kiasi cha shilling million 1,144,000  kwa mujibu wa mkuu wa shule hiyo ambazo Ndugu Kambarage amesema atazitoa ili kufikia jumatano ijayo maji yaweze kufikishwa shuleni hapo.

Hotuba ya mgeni rasmi
Mkuu wa shule ya sekondari Kunzugu Nyaeri  Suzan Mwisawa. Picha Adelinus Banenwa

Kupitia  taarifa ya shule mkuu wa shule ya sekondari Kunzugu Nyaeri  Suzan Mwisawa amesema katika shule hiyo  maafali hiyo ni ya 16 tangu shule kuanzishwa mwaka 2005 huku akibainisha changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo ni pamoja na utoro kwa wanafunzi samani za ofisini maji ambapo kipaumbele cha shule kwa sasa ni suala la maji.

Taarifa ya mkuu wa shule
Wahitimu wa kidato Cha nne Kunzugu Sekondari wakisoma risala, Picha na Adelinus Banenwa

Awali wakisoma risala mbele ya mgeni rasmi wanafunzi wa kidato cha nne wanaotarajia kuhitimu mwezi ujao wamesema walianza shule wakiwa wanafunzi 179 huku waliobahatika kufika leo ni 127 huku wengine wakishindwa kufikia leo kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na utoro kuhama na ujauzito.

Risala ya wahitimu