Mazingira FM

Wawili wajeruhiwa na mamba siku ya Chrismas Bunda

27 December 2023, 12:51 pm

Watu wawili wamenusurika kifo baada ya kushambuliwa na mamba siku ya tarehe 25 wakati wakiendele na shughuli zao katika ufukwe wa ziwa Victoria.

Na Adelinus Banenwa

Watu wawili wamenusurika kifo baada ya kushambuliwa na mamba siku ya tarehe 25 wakati wakiendele na shughuli zao katika ufukwe wa ziwa Victoria.

Afisa tarafa wa tarafa ya Kenkombyo ndugu Boniphas Maiga amewataja manusura watukio hilo kuwa ni Debora Mganga (46) na Mfungo Magoma (48) wote wakazi wa Kijiji Cha Mayoro kata ya Nyamihoro Halmashauri ya Wilaya ya Bunda mkoani Mara.

Aidha Afisa tarafa ameongeza kuwa watu hao walishambuliwa na mamba katika maeneo mawili tofauti na wamelazwa kituo cha afya cha Kasahunga wakiendele na matibabu huku Debora akitajwa kuendelea vizuri na Mfungo akitajwa hali yake kuwa siyo nzuri kwa kuwa Mamba huyo amemjeruhi sehemu za siri.

Maiga amesema kufuatia mfululizo wa matukio ya watu kukamatwa na mamba ameazimia kuitisha mikutano Kwa wakazi wote wanaoishi kandokando mwa ziwa Victoria ili kuwapa elimu ya kuacha kwenda kwenye maeneo hayo.

Sauti ya Afisa tarafa wa tarafa ya Kenkombyo ndugu Boniphas Maiga