Mazingira FM

kutozingatia vipimo sahihi ndo changamoto ya upungufu wa Dawa kwa wakulima wa Pamba Bunda: Mwanri

15 March 2022, 5:27 pm

balozi wa Pamba nchini Tanzania Mh Agrey Mwanri Akimpongeza mkulima aliyelima kwa kuzingatia mstari na vipimo sahihi

Balozi wa Pamba nchini Tanzania Mh Agrey Mwanri amesema wakulima wa Pamba wamekuwa na malalamiko kuhusu upungufu wa Dawa kutokana na maeneo ya mashamba yao kutokuwa na vipimo sahihi

Kauli hiyo ameitoa Leo 15 march 2022 katika siku ya tatu ya ziara yake kwa wakulima wa Pamba Wilayani Bunda ambapo amesema kwa utafiti chupa Moja ya sumu inatosha kwa ekari moja ya Pamba

Mwanri amesema amekutana na malalamiko mengi kwa wakulima kuwa dawa haitoshi chupa Moja kwa ekari lakini baada ya kufuatilia mashamba hayo yanakuwa ni zaidi ya ekari hivyo kwa dawa hizo ni ngumu kutosha
Balozi Mwanri ameongeza kuwa tatizo la dawa kutofanya kazi ya kuua wadudu inatokana na wakulima kutofuata maelekezo sahihi ya upuliziaji sahihi wa dawa ikiwa ni pamoja na muda wa kupinga dawa, Aina ya vichwa vya pampu wanazozitumia wakati wa upuliziaji, namna ya uchanganyaji wa dawa hizo miongoni mwa sababu zingine

Pia amewashukuru viongozi wa Wilaya ya Bunda na mkoa wa Mara kwa ujumla kwa mwitikio waliouonyesha kwenye kilimo Cha Pamba kwa kutumia mstari wakati alipofikika kwenye shamba lenye ekari 3 la mkuu wa Wilaya ya Bunda Mh Joshua Nassar lililoko mtaa wa tairo kata ya Guta Halmashauri ya Mji wa Bunda

Kwa upande wake Adelina Mfikwa afisa kilimo Halmashauri ya Mji wa Bunda amesema baada ya semina ya kwanza iliyofanywa na Balozi huyo mwezi November mwaka Jana kuelekeza namna ya kupanda mbegu za Pamba kwa mstari wananchi wamekuwa na mwitikio mkubwa na wamefuata maelekezo aliyoyatoa

Ameongeza kuwa Halmashauri ya Mji wa Bunda imepangiwa kuzalisha Tani elfu 20 za Pamba kwa mwaka huu na kutokana na mwitikio mkubwa wa wakulima wanaimani watafanikiwa

Ametoa wito kwa wakulima kuzingatia elimu walioipata kutoka kwa balozi ya namna ya unyunyiziaji wa viuadudu kwa kuwa hiyo itawasaidia kupata mazao Bora na ya uhakika