Mazingira FM

Kituo cha afya Bunda chadaiwa kuwatoza fedha wajawazito, watoto

17 February 2024, 11:07 pm

Kituo cha Afya Bunda

Wananchi wamelalamikia kituo cha afya bunda kuwatoza fedha akina mama wanaokwenda kujifungua na watoto chini ya miaka mitano kinyume na sera ya afya.

Na Adelinus Banenwa

Wananchi wamelalamikia kituo cha afya Bunda kuwatoza fedha akina mama wanaokwenda kujifungua na watoto chini ya miaka mitano kinyume na sera ya afya.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara wa Mkurugenzi wa mji wa Bunda  iliokuwa na lengo la kusikiliza kero za wananchi katika kata ya Nyasura ambapo wamesema imekuwa ni desturi Kwa   baadhi ya watumishi ambao siyo waadirifu wamekuwa wakiwatoza wanawake wajawazito na watoto chini ya miaka mitano fedha kinyume na sera ya afya inayosema wanawake wajawazito na watoto wanatakiwa kupata huduma bure katika hospitali za umma.

Wananchi hao pia wameshangaa watumishi hao kutochukuliwa hatua zozote za kisheria na kinidhamu licha ya malalamiko ya wananchi ya mara kwa mara.

Afisa utumishi halmashauri ya mji wa Bunda akijibu baadhi ya kero za wanachi katika mkutano wa hadhara kata ya Nyasura, Picha na Adelinus Banenwa

Kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji halmashauri ya mji wa Bunda afisa utumishi aliwatoa hofu wananchi na kusema kuwa kero hiyo ameichukua na atakwenda kukutana na hao watumishi ili kujua kwa nini wanafanya hivyo angali wakijua huduma hizo zinatolewa bure pia huwenda wanafanya jambo amabalo hawalifahamu.

Aidha amewataka wananchi kuepuka kutengeneza mianya ya rushwa kwa watumishi badala yake wafuate utaratibu unavyotaka wakati wa kupata huduma mbalimbali.

Katibu wa siasa na uenezi CCM wilaya ya Bunda ndugu Gasper Charles, Picha na Adelinus Banenwa

Ziara hiyo imekuja ikiwa ni siku moja baada ya katibu wa siasa na uenezi CCM wilaya ya Bunda ndugu Gasper Charles kupitia baraza la madiwani halmashauri ya mji wa bunda kuagiza madiwani na watumishi wa halmashauri kufanya mikutano ya hadhara ili kusikiliza na kutatua kero za wananchi badala ya kusubili viongo wa ngazi za juu.

katibu wa siasa na uenezi CCM wilaya ya Bunda ndugu Gasper Charles