Mazingira FM

Kambarage Wasira: achangia laki tano kumaliza uhaba wa matundu ya vyoo bunda sekondari.

14 April 2023, 8:26 pm

Ndugu Kambarage wasira atoa shilingi laki tano kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo kwenye mabweni shule ya sekondari Bunda

katika risala ya mkuu wa shule hiyo mwalimu Charles Somba mbele ya mgeni rasmi katika maafali ya nane ya kidato cha sita yaliyofanyika leo 14 April 2023 ambapo jumla ya wanafunzi 126 wamehitimu  kati yao wasichana 71 na wavulana 55.

Kupitia risala hiyo mkuu wa shule amezibainisha changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na upungufu wa matundu ya vyoo kwa wasichana wa bweni, upungufu wa mabweni, ukosefu wa makitaba pamoja na ukosefu wa maji ya uhakika

Aidha mwalimu Somba amesema kati ya changamoto hizo ukosefu wa choo ya wasichana wa bweni ndilo jambo muhimu kushughulukiwa kwa sasa kutokana na umuhimu wake ambapo kiasi cha shilingi milioni tatu na laki sita (3,600,000)  kinaitajika kujenga jumla ya matundu manne (4) ya vyoo.

Charles Somba

Aidha ndugu Magwa Philipo Malala   kwa niaba ya mgeni rasmi Kambarage Wasira katika maafali hiyo  amechangia kiasi cha shilingi laki tano huku akiwataka wazazi na walezi kushirikiana na uongozi wa shule kuhakikisha changamoto hiyo inatatuliwa.

Magwa philipo