Mazingira FM

239 wahitimu uwalimu Bunda ngazi ya stashahada

24 April 2026, 7:01 am

Baadhi ya wanafunzi waliohitimu masomo yao ngazi ya stashahada ya uwalimu

Mkuu wa chuo cha uwalimu Bunda mwal Venance Mwita Mancheye amewahasa wahitimu kujiendeleza kielimu kwa kuwa ujifunzaji hauna mwisho, kusoma kompyuta na kuwa na heshima kwa kila mtu.

Na Adelinus Banenwa

Jumla ya wanafunzi wa chuo cha uwalimu Bunda 239 katika tahasusi tatu wamehitimu masomo yao ngazi ya stashahada ya uwalimu  huku 133 kati yao wakiwa ni wasichana  na 106 wakiwa ni wavulana.

Mkuu wa chuo cha uwalimu Bunda mwal Venance Mwita Mancheye amesema kama chuo wanayo imani kubwa kwa wahitimu hao Kwenda kufanya vizuri shughuli zao za kufundisha kutokana ana kupikwa vizuri

Mkuu wa chuo cha uwalimu Bunda mwal Venance Mwita Mancheye

Aidha amewahasa wahitimu hao kujiendeleza kielimu kwa kuwa ujifunzaji hauna mwisho, kusoma kompyuta na kuwa na heshima kwa kila mtu miongoni mwa mambo mengine.

Sauti ya Mkuu wa chuo cha uwalimu Bunda mwal Venance Mwita Mancheye
Lukas Daniel Marco makamu mwenyekiti halmashauri ya mji wa Bunda akikabidhi kiasi cha shilingi milioni moja

Kwa upande wake Lukas Daniel Marco ambayeni makamu mwenyekiti halmashauri ya mji wa Bunda kwa niaba ya mgeni rasmi Ester Amos Bulaya mbunge wa jimbo la Bunda mjini akijibu risala ya wahitimu wa chuo hicho amesema mgeni rasmi ametoa shilingi million 1 kwa ajili ya kurekebisha sehemu ya kunawia wakati wa kupata chakula huku akitoa ahadi ya kusaidia vifaa vya michezo katiaka chuo hicho ambavyo ni mipira 5 na jezi .

Sauti ya Lukas Daniel Marco makamu mwenyekiti Bunda TC

Mahafali hay oni ya 40 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho huku yakiwa ni mahafali ya kwanza tangu kuanzishwa kwa mtaala mpya wa elimu wa mwaka 2014  toleo la 2023