Mazingira FM

Mama lishe ageuka nguzo ya familia kupitia madini

25 July 2026, 9:48 pm

Monica Filimoni mchimbaji Mgodi wa Walwa

Wanawake wengi wanaofanya kazi migodini wanajihusisha na shughuli halali za kujipatia kipato, kinyume na mtazamo wa baadhi ya watu.

Na Edward Lucas

Uwezeshaji wa wanawake kupitia shughuli za uchimbaji madini umetajwa kuwa miongoni mwa njia zinazowasaidia kujikwamua kiuchumi na kuongeza ushiriki wao katika kugharamia mahitaji ya familia.

Hali hiyo imejidhihirisha kwa Monica Filimoni wa Mgodi wa Walwa uliopo Kinyambwiga, Wilaya ya Bunda, ambaye ametoka kuwa mama lishe hadi kumiliki mashine za kuchakata madini, maduara ya uchimbaji na mwalo wa kukamatia madini.

Sauti ya Monica Filimoni

Monica anasema hatua hiyo ilimpa ujasiri wa kuendelea kuwekeza katika shughuli za uchimbaji, jambo lililomwezesha kupanua shughuli zake na kumiliki vifaa pamoja na maeneo yake ya uzalishaji.

Sauti ya Monica Filimoni
Mgodi wa Walwa ambapo Monica anafanya shughuli zake

Anasema mafanikio hayo yameongeza uwezo wake wa kuchangia mahitaji ya familia na kumpunguzia utegemezi wa kifedha aliokuwa nao awali.

Sauti ya Monica Filimoni

Makamu Mwenyekiti wa Wachimbaji wa Madini Wilaya ya Bunda, Malack Silas, amesema mafanikio ya wanawake kama Monica yanadhihirisha kuwa wanawake wengi wanaofanya kazi migodini wanajihusisha na shughuli halali za kujipatia kipato, kinyume na mtazamo wa baadhi ya watu wanaodhani kuwa uwepo wao migodini unahusishwa na ukahaba pekee

Sauti ya Malack Silas

Kwa mujibu wa uongozi wa mgodi wa Walwa, wanawake wameendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali za uchimbaji na uchakataji wa madini huku mgodi ukiweka sheria na taratibu za kulinda usalama wa wachimbaji wote.

Wadau wa maendeleo wanasema kuwa kuwawezesha wanawake kiuchumi ni miongoni mwa hatua zinazoweza kuongeza ustawi wa familia na kupunguza mazingira yanayoweza kuchangia ukatili wa kijinsia.