Mazingira FM

Mtanda aipongeza halmashauri ya Bunda TC ubora wa miradi

22 September 2023, 5:25 pm

Mkuu wa mkoa wa Mara mhe Said Mohamed Mtanda, Picha na idara ya habari Bunda TC

Mkuu wa mkoa wa Mara mhe Said Mohamed Mtanda ameipongeza halmashauri ya mji wa Bunda kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo kwa viwango na kasi inayoitajika.

Na Adelinus Banenwa

Mkuu wa mkoa wa Mara mhe Said Mohamed Mtanda ameipongeza halmashauri ya mji wa Bunda kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo kwa viwango na kasi inayoitajika.

Mtanda ameyasema hayo Sept 20, 2023 katika ziara yake wilayani Bunda wakati akikagua miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa ndani ya halmashauri ya mji wa Bunda.

Ujenzi wa shule ya Sekondari Bunda mjini, Picha na idara ya habari Bunda TC

Katika ziara hiyo Mhe Mtanda ametembelea na kukagua ujenzi wa shule ya sekondari ya Bunda mjini inayojengwa kata ya Bunda Stoo mtaa wa Migungani, pia ameutembelea mradi wa ujenzi wa hospitali ya halmashauri ya Mji wa Bunda inayojengwa kata ya Bunda Stoo mtaa wa Idara ya Maji.

Ujenzi wa hospital ya halmashauri ya mji wa Bunda, Picha na idara ya habari Bunda TC

Mhe Mtanda amesema mbali na mapungufu kidogo yaliyopo katika utekelezaji wa miradi hiyo ila ipo kwenye kiwango kinachoitajika.

Aidha mkuu huyo wa  mkoa amemuelekeza mkurugenzi mtendaji wa mji wa Bunda kuhakikisha anasimamia vizuri fedha za miradi hasa idara ya manunuzi ili kuepuka kununua vifaa kwa gharama za juu kuliko bei iliyoko sokoni