Mazingira FM
Mazingira FM
3 June 2026, 7:13 pm

Aidha Baraka amesema changamoto ya mabadiliko ya tabia ya nchi ikiwemo vipindi virefu vya jua na mvua vinasababisha uharibifu wa mazingira.
Na Adelinus Banenwa
Mifugo, mabadiliko ya tabia ya nchi na upungufu wa rasilimali bado ni changamoto kubwa katika kampeni ya utunzaji wa mazingira
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa BUFADESO Baraka Kamese kupitia Mazingira FM kwenye kipindi cha kilimo na mifugo ambapo ameeleza kuwa mara nyingi wao kama BUFADESO wamekuwa wakitoa miti kwa taasisi mbalimbali lakini changamoto kubwa imekuwa ni wachungaji wa mifugo kupeleka mifugo yao kwenye maeneo ya ambayo miti imepandwa
Aidha Baraka amesema changamoto ya mabadiliko ya tabia ya nchi ikiwemo vipindi virefu vya jua na mvua vinasababisha uharibifu wa mazingira .
Amesema kutokana ana hayo BUFADESO wameendelea kutoa elimu katika vikundi mbalimbali vya wakulima ikiwemo kushirikiana na serikali za halmashauri kupanda miti katika maeneo ya taasisi.