Mazingira FM

Ukosefu wa eneo la wazi chanzo cha ukosefu miradi Kata ya Bunda mjini

8 September 2023, 1:33 pm

Mhe Mzamili diwani wa kata ya Bunda Mjini, Picha na Adelinus Banenwa

Mhe Mzamili diwani wa kata ya Bunda Mjini amesema kata ya Bunda Mjini ina eneo Moja tu la wazi la miti mirefu linalipatikana mtaa wa Mapinduzi ambalo kisheria haliruhusiwi kubadirishiwa matumizi

Na Adelinus Banenwa

Imeelezwa kuwa ukosefu wa maeneo katika kata ya Bunda mjini iliyopo ndani ya halmashauri ya mji wa Bunda ndicho chanzo Cha ukosefu wa baadhi ya miradi ndani ya kata hiyo.

Hayo yamesemwa na diwani wa kata ya Bunda mjini Mzamili Ibrahim kirwanila katika mkutano wake na wananchi wa kata hiyo uliofanyika leo katika viwanja vya Sabasaba Mjini Bunda

Akitolea ufafanuzi wa ukosefu wa shule, zahanati na huduma zingine Mhe diwani amesema Mara kadhaa amekuwa akipata fedha Kwa ajili ya kujenga miundombinu hiyo ila changamoto imekuwa ni maeneo ya kujenga

Mhe Mzamili amesema kata ya Bunda mjini ina eneo Moja tu la wazi la miti mirefu linalipatikana mtaa wa mapinduzi ambalo kisheria haliruhusiwi kubadirishiwa matumizi

Ufafanuzi huu umekuja baada ya baadhi ya wananchi kuhoji juu ya hatua ya serikali kutumia fedha zilizokuja Kwa ajili ya kujenga shule ya Bunda mjini lakini wao wameijenga ndani ya kata nyingine?