Mazingira FM

CHADEMA: Baadhi ya AMCOS hatarini kufilisiwa Bunda

2 July 2023, 3:35 pm

Jacob Sospeter Maiga

Baadhi ya vyama vya ushirika AMCOS halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara viko kwenye hatihati ya kuuzwa mali zao ikiwa ni pamoja na maghala au stoo kutokana na mikopo ya matrekta kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo.

Haya yamebainishwa kupitia mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wilaya ya Bunda na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho kuelezea namna ambavyo jambo hilo limeibua taharuki miongoni mwa wakulima na kuiomba serikali kuingilia kati ili kunusuru mali za AMCOS hizo.

Akizungumzia suala hilo mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Bunda, Jacob Sospeter Maiga amesema miongoni mwa AMCOS zilizo katika hati hati ya kuuzwa mali zao ni pamoja na AMCOS ya Kunzugu na Balili.

Jacob Sospeter Maiga

Sambamba na hayo Maiga amebaini vituo ambavyo vinakumbwa na sakata hilo.

Jacob Sospeter Maiga

Kufuatia taarifa hizi Mazingira Fm imefika katika Ofisi za AMCOS kunzugu na Balili ili kupata uthibitisho wa taarifa hizi na hapa viongozi hao wanabinisha kile kinachoendelea juu ya taarifa hizo

Nyang’era Lukiko

Akifafanua zaidi maswali ya waandishi wa habari wa Radio Mazingira Fm, Nyang’era Lukiko amesema

Nyang’era Lukiko

Kwa upande wake Katibu wa AMCOS Balili, Samweli Chacha amesema

Samweli Chacha

Kufuatia taarifa hizi, Mazingira Fm imefanya juhudi za kumtafuta Afisa Ushirika Halmashauri ya Mji wa Bunda ili kupata ufafanuzi zaidi juu ya taarifa hizi lakini alieleza kuwa yuko mkoani kikazi na hivyo waandishi wetu wanaweza kumtembelea ofisini kwake siku ya jumatatu juu ya taarifa hizo.

Aidha Juhudi za kuwapata uongozi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania kwa ufafanuzi wa taarifa hizi kwa kutumia simu yao hazijazaa matunda hivyo Mazingira Fm inaendelea na juhudi za kuwapata viongozi hao kwa ufafanuzi zaidi.