Mazingira FM

Bunda yafanikiwa pakubwa 2023

22 December 2023, 8:06 am

Serikali wilayani Bunda imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto za wananchi katika sekta mbalimbali ikiwa ni kwa upande wa miundombinu, Elimu, Afya na Usuruhishi kwa kipindi cha mwaka 2023.

Na Adelinus Banenwa

Serikali wilayani Bunda imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto za wananchi katika sekta mbalimbali ikiwa ni kwa upande wa miundombinu, Elimu, Afya na Usuruhishi kwa kipindi cha mwaka 2023.

Hayo yamebainishwa na katibu tawala wilaya ya Bunda Salumu Halfani Mtelela kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Bunda Dr Vicent Naano wakati akizungumza na Mazingira fm ofisini kwake mapema leo.

Salumu amesema serikali wilayani Bunda chini ya mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dr Vicent Naano imefanikiwa kusimamia ujenzi wa barabara ya Nyamuswa, Bulamba kwa kiwango cha lami, Ujenzi wa hospitali za halmashauri, Ukamilishwaji wa chujio la maji Nyabehu miongoni mwa mafanikio mengine.

Katibu tawala kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Bunda amesema hali ya usalama iko vizuri kuelekea kipindi cha sikukuu za Chrismas na mwaka mpya.

Aidha amewataka wazazi na walezi kuweka umakini kwa watoto wao kuelekea kindi hiki cha sikukuu za kufunga mwaka ambapo pia amkiwataka madereva kujiepusha ma matumizi ya vileo wanapoendesha magari .