Mazingira FM
Mazingira FM
26 June 2026, 11:21 am

Wakizungumza baada ya kupokea fedha hizo baadhi ya wanufaika hao wamesema kuwa fedha hizzo zimewasaidia kupata mitaji,kukuza vipato vyao kutokana na n mkopo huo wenye masharti nafuu kutoka halmashauri.
Na Mariam Mrambi
Jumla ya vikundi 33 kutoka maeneo mbalimbali katika halmashuri ya wilaya ya bunda mkoani Mara vimepatiwa mkopo wa asilimia 10 wa halimashauri kwaajili ya wanawake vijana na wenye ulemavu wenye thamani ya shilingi Milioni 240
Akizungumza hii leo mkuu wa kitengo cha maendeleo ya yamii wa halmashauri hiyo Bi Oktvina Kiwone wakati wahafla ya kukabidhi mkopo huo amesema kuwa halmashuri ilitenga bajeti kwaajili ya kuviwezesha vikundi ambapo amewaasa wanufaika wa mkopo huo wautumie kwa kile walichokusudia na kuzirejesha kwa wakati
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bunda bwana George Mbilinyi amevipongeza vikundi hivyo kwa kupata fedha hizo na fedha hizo zinatolewa kwa uwazi bila kificho ambapo ametumia nafasi hiyo kuwaagiza maafsa maendeleo wa kata kuhakikisha wanavisaidia vikundi katika kutuima fedha hizo kwa miradi waliyolenga

Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bunda Renatus Mjungu Mjungu amesema kuwa fedha hizo zinatolewa ili watu wakazifanyie kazi za miradi waliyo kusudiwa na kwamba hiyo i fursa muhimu kwao
Wakizungumza baada ya kupokea fedha hizo baadhi ya wanufaika hao wamesema kuwa fedha hizzo zimewasaidia kupata mitaji,kukuza vipato vyao kutokana na n mkopo huo wenye masharti nafuu kutoka halmashauri
Akikabidhi fedha hizo katibu tawala wa wilaya ya Bunda Salum Halfan Mtelela kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya bunda ameipongeza halmashauri ya wilaya ya bunda kwa kazi nzuri ya usimamizi hadi kufikia hatua ya kugawa fedha hizo za vikundi
Aidha amewataka watu kuchangamkia fursa zinapotangazwa pia ameviasa vikundi vilivyopata fedha hizo wazitumie kwa malengo waliyo kusudiwa na wazirejeshe kwa wakati kwani fedha hizo zilizotolewasiyo sadaka