Mazingira FM

Lightness aibuka mshindi Tsh 1.mil kampeni ya YAS

31 July 2026, 9:18 pm

Meneja wa Yas Kanda ya Mara Kusini, Halid Omary

Hafla ya kukabidhi hundi ya mshindi huyo imefanyika katika ofisi za Yas zilizopo mtaa wa FM, mjini Mugumu, Wilaya ya Serengeti, Mkoa wa Mara.

Na Adelinus Banenwa

Katika kuendelea kudhihirisha ubora wa huduma zake na kuwazawadia wateja wake, kampuni ya mawasiliano ya Yas Kanda ya Mara Kusini imekabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni moja kwa mshindi wa kampeni ya “Ikiingia Tu Goli”, kampeni maalumu iliyoendeshwa wakati wa michuano ya Kombe la Dunia.

Mshindi wa zawadi hiyo, Lightness Mushi, mkazi wa Wilaya ya Serengeti, amesema hakutarajia kuwa mshindi wa kampeni hiyo. Amesema alipigiwa simu kutoka namba 100, lakini mwanzoni hakupokea akidhani ni simu ya kawaida. Baada ya kupigiwa kwa mara ya pili ndipo alipokea na kupewa taarifa kuwa amejishindia shilingi milioni moja.

Sauti ya Lightness Mushi

Aidha, Lightness amewahimiza wateja wa Yas kutopuuza kampeni mbalimbali zinazoendeshwa na kampuni hiyo, akisema ni za kweli na zinawanufaisha wateja wengi.

Mshindi wa zawadi ya ikiingia tu goli, Lightness Mushi

Kwa upande wake, Meneja wa Yas Kanda ya Mara Kusini, Halid Omary, amesema kampeni ya “Ikiingia Tu Goli” ilihitimishwa Julai 30 kwa kuwa ilikuwa maalumu kwa kipindi cha michuano ya Kombe la Dunia. Amesema wanafurahia kumpata mshindi kutoka Wilaya ya Serengeti ambaye amejishindia shilingi milioni moja kama zawadi ya droo ya kila siku ya kampeni hiyo.

Halid ameongeza kuwa Yas itaendelea kuandaa kampeni mbalimbali zenye manufaa kwa wateja wake, huku akiwakaribisha Watanzania wanaotumia mitandao mingine kujiunga na Yas ili kunufaika na ofa na huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo.

Sauti ya Meneja wa Yas Kanda ya Mara Kusini, Halid Omary

Hafla ya kukabidhi hundi ya mshindi huyo imefanyika katika ofisi za Yas zilizopo mtaa wa FM, mjini Mugumu, Wilaya ya Serengeti, Mkoa wa Mara.