Mazingira FM

Wakazi wa Bunda kilio kukatika kwa maji

19 August 2026, 10:20 am

Bomba la maji ambalo linaonesha halijatoa maji muda mrefu

Wanaiomba serikali iweze kuingilia kati suala hili ili waweze kupata maji safi na salama kwa wakati muafaka

Na Juma Hangi

Wakazi  wa  Bunda Mjini  wamelalamikia   kukatika kwa huduma ya maji kwa  siku nne hadi wiki nzima, wakisema hali hiyo inakwamisha shughuli za uzalishaji Pamoja  na matumizi ya kawaida  ya  nyumbani.

Wakizungumza  leo, Agosti 18, 2026, wakazi hao wameiomba serikali na mamlaka husika kuchukua hatua za haraka kukabiliana na changamoto hiyo, wakisisitiza kuwa maji ni uhai na bila maji shughuli nyingine za kila siku zinakwama.

wanaiomba serikali iweze kuingilia kati suala hili ili waweze kupata maji safi na salama kwa wakati muafaka,nawengine wakichukizwa na hali hii nakutaka hata kuondoa mabomba nakuchimba visima ili waweze pata huduma hii ya maji safi na salama kwa uhakika nakuachana na masuala ya mabomba

Aidha wameiomba  mamlaka  zinazohusika  kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu sababu ya kukatika kwa maji na hatua zinazochukuliwa,  huku wakitaka  huduma  hiyo  kurejeshwa na kupatikana  kwa uhakika.

Sauti za baadhi ya wakazi wa mji wa Bunda