Mazingira FM

RUPA Memorial hospital kutoa huduma za kibingwa hasa kwa akina mama saa 24

18 February 2024, 5:14 pm

Askofu wa kanisa Katoliki jimbo la Bunda Saimon Chibuga  Masondole, akiwa na viongozi wa RUPA memoria hospital wakati wa utiaji baraka wa hospitali hiyo ili ianze kutoa huduma, Picha na Adelinus Banenwa.

Askofu wa kanisa Katoliki jimbo la Bunda Saimon Chibuga  Masondole amewataka matabibu kufanya kazi kwa moyo kwa kuwa Mungu amewapa karama ya uponyaji.

Na Adelinus Banenwa

Askofu wa kanisa Katoliki jimbo la Bunda Saimon Chibuga  Masondole amewataka matabibu kufanya kazi kwa moyo kwa kuwa Mungu amewapa karama ya uponyaji.

Askofu Masondole ameyasema hayo wakati wa kubariki na kufungua huduma za matibabu katika hospitali ya RUPA Memorial hospital iliyopo eneo la Majengo kata ya kabarimu Mjini Bunda.

RUPA Memorial hospital, Picha na Adelinus Banenwa

Naye Professor Charles Majinge ambaye ni Mkurugenzi Mkuu na mmiliki wa hospitali hiyo amesema wameamua kuanzisha hospital lengo ni kutoa huduma ambazo zitawezesha wagonjwa kupata msaada wa matibabu ya kibingwa.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa hospital hiyo David Majinge amesema hospital hiyo inatoa huduma zote kwa watoto, wanawake na wanaume na ameongeza kuwa Kwa Sasa yupo daktari Bingwa na mbobezi  wa magonjwa ya wanawake hivyo kwa wanawake wote wenye changamoto ya mbalimbali wafike ili kupatahuduma.

Baadhi ya wagonjwa wakisubiri huduma RUPA hospital, Pacha na Adelinus Banenwa.

Kwa upande wao baadhi ya wagonjwa waliofika kutibiwa kwa mara ya kwanza katika hospitali hiyo wamesifu huduma zinazotolewa kuanzia ngazi ya mapokezi, vipimo, ushauri na hata matibabu.