Bunda; Nymakokoto wafanya usafi kiwilaya
1 January 2023, 6:26 pm
Diwani wa kata ya Nyamakoko Mhe Emanuel Machumu Malibwa amewashukuru wananchi waliojitokeza kufanya usafi katika maeneo mbalimbali katika kata hiyo
Akizungumza na Mazingira Fm mara baada ya zoezi hilo la ufasi Mhe Malibwa amesema alipokea maelekezo juu ya kata yake kuwa mwenyeji wa kufanya usafi kwa Halmashauri ya Mji wa Bunda kama ilivyo kawaidi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi kufanyika usafi kote nchini
Diwani Malibwa amesema pamoja na maeneo yaliyofanyiwa usafi pia walifika kituo Cha Polisi Wilaya ili kushirikiana na maofisa wa polisi kukifanyia usafi kituo hicho ambacho pia kinapatikana katika kata hiyo.
Naye mwenyekiti wa wajasiriamali Mkoa wa Mara Charles Waitala amesema Machinga na wajasiriamali kwa ujumla ndiyo wazalishaji wakubwa wa taka hivyo jambo la kufanya usafi kwenye maeneo Yao ni jambo la kuzingatia sana na serikali ilitoa maelekezo juu ya kufanya usafi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi hivyo ni wajibu wao kufanya hivyo
Nao Baadhi ya wananchi waliojitokeza kufanya usafi akiwemo mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM kata ya Nyamakoko amesema tofauti na zamani Leo Vijana wamejitokeza kwa wingi kwenye zoezi la usafi na amewaasa waendelee kujitoa katika shughuli zingine za maendeleo katika kata hiyo.