Walimu Nyaburundu watajwa kujiingiza kwenye siasa shuleni
18 October 2023, 12:18 pm
Imeelezwa kuwa baadhi ya walimu wa shule ya Msingi Nyaburundu iliyopo kata ya Ketare halmashauri ya wilaya ya Bunda mkoani Mara wamejiingiza katika siasa na kusahau wajibu wao shuleni.
Na Thomas Masalu
Imeelezwa kuwa baadhi ya walimu wa shule ya Msingi Nyaburundu iliyopo kata ya Ketare halmashauri ya wilaya ya Bunda mkoani Mara, wamejiigiza katika siasa na kusahau wajibu wao shuleni.
Hayo yameelezwa na wakazi wa Kijiji hicho mbele ya kaimu Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Bunda katika mkutano wa hadhara, uliofanyika jumanne 17 Oct 2023 shuleni hapo.
Wakazi hao wamesema, wamechoshwa na tabia za walimu hao kuendekeza siasa shuleni wakati wameaminiwa na serikali kufundisha watoto na si vinginevyo.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Ketare, mheshimiwa Mramba Simba Nyamkinda amesema ni muda mrefu wakazi wa Nyaburundu wamekuwa wakialamika juu ya mwenendo wa walimu hao hasa katika kuchanganya siasa shuleni.
Mramba amesema hata miradi inayopelekwa shuleni hapo, baadhi ya walimu wanaeneza maneno kuwa miradi hiyo ni ya mtu binafsi na siyo serikali iliyopo madarakani.
Hata hivyo kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Bunda ndugu Oscar Jeremiah Ncheye amesema ameyapokea yote na ameahidi kuyafanyia kazi.
Ncheye amesema ni kinyume cha sheria mtumishi kujihusisha na siasa kama mtumishi anataka kufanya shughuli hiyo basi vyema akaacha kazi na akajielekeza huko.