Mazingira FM

BUWSSA: Wizi wa maji Bunda haukubaliki

11 September 2023, 5:25 pm

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Bunda BUWSSA Bi Esther Giryoma. Picha na Adelinus Banenwa

Tatizo la wizi wa maji ndani ya mji wa Bunda lipo na wanaendelea kukamata watu wote wanaojihusisha na wizi huo pia mamlaka haipendezwi na tabia hizo.

Na Adelinus Banenwa

Wito umetolewa kwa wananchi wilayani Bunda mkoani Mara kuacha tabia ya wizi wa maji kutoka Mamlaka ya Maji Bunda BUWSSA badala yake watumie njia sahihi kuomba kupatiwa huduma ya maji majumbani mwao.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa mamlaka ya maji Bunda BUWSSA Bi Esther Giryoma katika kipindi cha Asubuhi leo ndani ya  radio Mazingira Fm leo ambapo amesema tatizo la wizi wa maji ndani ya mji wa Bunda lipo na wanaendelea kukamata watu wote wanaojihusisha na wizi huo pia mamlaka haipendezwi na tabia hizo akitaja kuwa wizi wa maji ni ushamba.

Aidha akifafanua kuhusu suala la ankara ya maji kuwa juu kwa mji wa Bunda Bi Esther amesema mpango wa BUWSSA kwa sasa ni kuwaunganisha watu wengi ili ankara ya maji iweze kupungua.