Mazingira FM

BUWSSA yapewa kongole usimamizi wa miradi ya maji

12 November 2023, 12:36 pm

Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dr Vicent Naano

Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dkt. Vicent Naano ameipongeza Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Bunda kwa ubora wa miradi wanayoitekeleza.

Na Adelinus Banenwa

Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dkt. Vicent Naano ameipongeza Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Bunda BUWSSA kwa ubora wa miradi wanayoitekeleza.

Dc Naano ameyasema hayo katika ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa na BUWSSA ndani ya mji wa Bunda lenye lengo la kupunguza changamoto ya huduma ya maji kwa wananchi.

Mkurugenzi wa a mamlaka ya maji Bunda Esther Giryoma.

Miongoni mwa miradi iliyotembelewa ni pamoja na mradi wa manyamanyam,a mugaja unaogharimu shilingi 1.1 bilion ambao ukikamilika utawanufaisha zaidi ya wakazi elfu tano, pamoja na mradi wa balili rubana na kunzungu unaogharimu zaidi ya shilingi 700 milion.

Dc naano amesema serikali inatoa fedha nyingi katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma mbalimbali huku akiipongeza BUWSSA kwa usimamizi mzuri wa miradi wanyoyoitekeleza achini ya mkurugenzi wa a mamlaka hiyo Esther Giryoma.