Mazingira FM

Dkt. Samia awataka wanabunda kutafakari maamuzi ya kisiasa

10 October 2025, 8:54 am

Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan akioneshana jambo na makamu mwenyekiti chama cha mapinduzi Tanzania bara Stephan Wasira

Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka Wananchi wa Bunda kutafakari kabla ya kufanya maamuzi ya kisiasa.

Na Adelinus

Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka Wananchi wa Bunda kutafakari kabla ya kufanya maamuzi ya kisiasa, huku akisisitiza kwamba uongozi wa nchi unahitaji uzoefu na uwezo wa kusimamia masilahi ya wananchi.

Akizungumza katika Mkutano wa Kampeni uliofanyika leo octoba 09, 2025, katika Wilaya ya Bunda, Mkoa wa Mara, Dkt. Samia amesema uendeshaji wa nchi hakuna majaribio, hivyo ni muhim wananchi kuendelea kuamini Chama chenye uzoefu wa kuongoza Serikali.

Baadhi ya wakazi wa Bunda waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni za mgombea urais kupitia chama cha Mapinduzi wilayani ya Bunda

Dkt. Samia bado anaendelea na Kampeni za Chama Cha Mapinduzi katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, ambapo leo ni zamu ya Wananchi wa Mkoa wa Mara kusikiliza sera na ahadi za Mgombea huyo.

Sauti ya Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan

Awali akizungumza katika mkutano huo mgombea ubunge wa jimbo la Bunda mjini kwa tiketi ya CCM Esther Bulaya amesema endapo Dkt Samia akichaguliwa anaomba kushughulikiwa mambo kadhaa ikiwemo, kutekelezwa kwa mradi wa TACTIC, usambazaji maji kwa mji wa bunda na kutoa huduma bure za afya kwa akina mama wajawazito, watoto na wazee.

Sauti ya mgombea ubunge wa jimbo la Bunda mjini kwa tiketi ya CCM Esther Bulaya