Mazingira FM

Mbunge Maboto: Awahimiza Bunda Mjini kushiriki Sensa kikamilifu

23 August 2022, 7:32 am

Mbunge Jimbo la bunda Mjini Mhe Robert Chacha Maboto amewahimiza wakazi wa Jimbo la Bunda Mjini kushiriki Sensa ya watu na makazi kikamilifu

Akizungumza na redio Mazingira Fm Mhe Maboto amesema lengo kuu la sensa ya watu na makazi ni kuisadia Serikali kupata idadi kamili ya watu wake ili iweze kupanga mipango ya maendeleo

Aidha ameongeza kuwa zipo dhana nyingi watu walizonazo kuhusu kuhesabiwa kama Mila na Imani lakini Imani hizo ni potofu wananchi watoe ushirikiano kwa makalani watakaofika kwenye kaya zao

“Nadhani tunapaswa kuachana na Mila potofu zinazotaja kwamba kuhesabiwa haitakiwi badala yake tuhakikishe tunahesabiwa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu”

Aidha Mhe Maboto amebainisha kuwa tangu achaguliwe kuwa mbunge Jimbo la Bunda Mjini miezi ishirini ameshatumia shilingi million 200 ambazo zimekwenda katika shughuli za maendeleo kwa wananchi ikiwepo kwenye vikundi vya wasiliamali kama ambavyo aliahidi kwenye kipindi Cha kampeini kwamba atatumia mshahala wake kuurudisha kwa wananchi