Mazingira FM

Wakazi Nyamakokoto watakiwa kununua milango 15 iliyoibwa shule za Balili, Bunda

21 June 2023, 10:31 am

Emmanuel Malibwa

Diwani wa kata ya Nyamakokoto Emmanuel Malibwa amewataka wakazi wa kata hiyo kuchangia utengenezaji wa milango 15 ya vyoo iliyoibwa katika shule za msingi za Balili na Bunda.

Akizungumza na radio Mazingira Fm katika kutamatatisha ziara yake ndani ya mitaa minne amesema tukio la wizi wa milango 15 ya vyoo katika shule za msingi za Balili na Bunda ni la ajabu na kwa kuwa wananchi waliona wizi huo unafanyika na hawakuchukua hatua sasa ni vema wakainunua.

Amesema serikali ilitoa fedha za ujenzi wa vyoo ambapo wananchi hawakuchangia chochote sasa kwa kuwa hawakuona uchungu, serikali haiwezi tena kutoa fedha kununua milango mingine na yeye kama diwani hayuko tayari kuona watoto wanapata shida, basi wazazi watawajibika kuitengeneza milango hiyo.

Emmanuel Malibwa

Aidha Mhe Malibwa amesema katika ziara yake ndani ya mitaa minne inayounda kata ya Nyamakokoto changamoto kubwa aliyokutana nayo ni suala la usalama ambapo amebainisha kuwa wenye nyumba kupangisha wapangaji wasiokuwa waaminifu hivyo ametoa maelekezo kwa wenye nyumba wote kata ya Nyamakokoto ni marufuku kumpangisha mtu asiyekuwa na kibali kwa maana ya barua ya mwenyekiti anakotoka ikiwa na mhuri na namba za simu.

Emmanuel Malibwa