Mazingira FM

Kamati ya Siasa CCM Bunda Stoo yaipongeza serikali miradi ya elimu na afya

29 January 2024, 3:06 pm

Wajumbe wa kamati ya Siasa kata ya Bunda stoo katika mradi wa shule mpya ya Msingi inayoitwa shule ya msingi Bunda stoo. Picha na Adelinus Banenwa.

Mwenyekiti wa ccm kata ya bunda stoo Charlse Mwita Chacha ameiomba serikali kupitia wataalamu wake kuchukua hatua madhubuti kukamilisha miradi Bunda stoo.

Na Adelinus Banenwa

Mwenyekiti wa ccm kata ya bunda stoo Charlse Mwita Chacha ameiomba serikali kupitia wataalamu wake kuchukua hatua madhubuti kukamilisha miradi mbalimbali inayotekelezwa katika kati hiyo ili wananchi waweze kupata huduma.

Mwenyekiti ameyasema hayo katika ziara ya kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi CCM iliyofanyika leo iliyokuwa na lengo la kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika kata hiyo.

Katika ziara hiyo kamati ya siasa imetembelea na kukagua hospitali ya halmashauri ya mji wa Bunda, shule za msingi za Bunda stoo, Migungani Bigutu pamoja na Miembeni.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Bunda stoo ndugu  Flavian Chacha amesema yeye kama mwakilishi wa wananchi wa kata ya Bunda stoo anafanya kila jitihada kuhakikisha miradi iliyoanzishwa ndani ya kata yake inakamilika.

Akisoma taarifa ya ujenzi  wa hospitali ya halmashauri moja ya madaktari anayesimamia ujenzi huo amesema jengo la wagonjwa wa nje  limefikia asilimia 95 na wanatarajia ifikapo mwezi wa pili mwaka huu waanze kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje yaani OPD.