Mazingira FM

Mkurugenzi radio Mazingira atoa msaada wa baiskeli kwa mtoto mwenye ulemavu

28 August 2023, 5:04 pm

Mkurugenzi wa radio Mazingira Fm ambaye pia ni diwani wa kata ya Ketare Mhe Mramba Simba Nyamkinda, Picha na Thomas Masalu

Mkurugenzi wa radio Mazingira Fm Mhe Mramba Simba Nyamkinda amemkabidhi baiskeli ya watu wenye ulemavu yenye thamani ya shilingi laki nne, kwa Zitto Alphonce ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Kiroreli kata ya Nyamang’uta halmashauri ya wilaya ya Bunda.

Na Thomas Masalu

Mkurugenzi wa radio Mazingira Fm ambaye pia ni diwani wa kata ya Ketare Mhe Mramba Simba Nyamkinda amemkabidhi baiskeli ya watu wenye ulemavu yenye thamani ya shilingi laki nne, kwa Zitto Alphonce ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Kiroreli kata ya Nyamang’uta halmashauri ya wilaya ya Bunda.

Makabidhiano hayo yamefanyika nyumbani kwa diwani wa kata hiyo, Kiremba Irobi akiwa pamoja na Mwalimu wa shule hiyo Baraka John.

Akizungumza baada ya kukabidhi baskeli hiyo, Mheshimiwa Mramba amesema alipata ombi la kumsaidia mtoto huyo kupitia kwa diwani wa kata ya Nyamang’uta.

Kwa upande wake bibi wa mtoto huyo Frolar Minja amemshukuru Mhe Mramba kwa kumsaidia mjukuu wake jambo ambalo ni hatua kubwa kwake na litamsaidia kufikia ndoto zake.