Mazingira FM
Mazingira FM
10 October 2025, 12:23 pm

Dkt. Charles ameonya tabia ya kutumia dawa za macho za maji bila ushauri wa kitaalamu,ataja madhara yanayoweza kutokea kama presha ya macho.
Na Catherine Msafiri
Katika jitihada za kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kutunza afya ya macho, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Macho, Dkt. John Mpande Charles kutoka hospital ya rufaa ya kumbukumbu ya mwalimu Nyerere ameeleza changamoto mbalimbali zinazowakumba watu wengi kuhusu afya ya macho, na ametoa ushauri kwa umma juu ya namna bora ya kujikinga na matatizo ya macho.
Dkt. Charles ameonya kuhusu tabia ya kutumia dawa za macho za maji bila ushauri wa kitaalamu. Ameeleza kuwa dawa hizo zinaweza kusababisha madhara makubwa endapo zitatumika bila vipimo au ushauri wa daktari.
Amezungumza hayo leo alipofanya mahojiano kwenye kipindi cha kapu letu kinacholuka radio Mazingira FM akieleza kuhusu afya ya macho.
Aidha Dkt. Charles amewataka wazazi kuwa waangalifu zaidi na afya ya macho ya watoto wao , pia ametoa wito kwa jamii kufika hospitali au vituo vya afya pindi wanapohisi dalili yoyote isiyo ya kawaida machoni.
Hata hivyo amebainisha kuwa matatizo ya macho yanatibika kwa njia tofauti tofauti pindi mtu atakapofika kuwaona wataalamu.