Mazingira FM

Yowe haiui mtu bali watu ndiyo wanaoua

21 April 2026, 9:52 pm

Jonas Kaijage Msaidizi wa mkuu wa polisi jamii wilaya ya Bunda

Ipo sheria ya ukamataji ambayo inaelekeza ukamataji salama na pindi wananchi wanaoshiriki ulinzi shirikishi wakikamata muhalifu wanatakiwa kutoa taarifa.

Na Adelinus Banenwa

Wananchi watakiwa kutojichukulia sheria mkononi ikiwemo kuhusuka katika mauaji ya wahalifu kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria

Jonas Kaijage Msaidizi wa mkuu wa polisi jamii wilaya ya Bunda amesema ipo sheria ya ukamataji ambayo inaelekeza ukamataji salama na pindi wananchi wanaoshiriki ulinzi shirikishi wakikamata muhalifu wanatakiwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi ili kuendelea nataratibu za kumfikisha mahakamani baada ya Upelelezi

Kaijage ameongeza kuwa wananchi wanatakiwa mahakamani kutoa ushahidi ambao unaweza kuwatia hatiani watuhumiwa wa uhalifu akisisitiza kuwa kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa wanapowakamata watuhumiwa baadaye uwaona mtaani hali inayolalamikia jeshi la polisi kuwaachia watuhumiwa

Akitoa ufafanuzi wa kadhia hiyo Kaijage amesema kuna baadhi ya makosa hata ukimfikisha mtuhumiwa polisi au mahakamani wanapewa dhamana kwa kuwa ni sehemu ya haki ya kisheria ya mtuhumiwa katika baadhi ya makosa hivyo wananchi waondoe dhana kuwa ameachiwa badala yake wanakila sababu ya kuuliza na kwenda kutoa ushahidi mahakamani

Sauti ya Jonas Kaijage Msaidizi wa mkuu wa polisi jamii wilaya ya Bunda