Mazingira FM

Watoto 1103 wamepata ujauzito ndani ya miezi minne Bunda

10 December 2023, 11:58 am

Katika kipindi  cha miezi minne ya julay hadi October  2023  watoto  712 kutoka halmashauri  ya wilaya ya Bunda na 391 kutoka  halmashauri ya mji wa Bunda wamepata ujauzito huku watatu kati yao wakiwa na umri chini ya miaka 14.

Na Adelinus Banenwa

Chart inayoonesha hali ya mimba za utotoni Kwa miaka mitatu ndani ya wilaya ya Bunda

Hayo yamebainishwa na ofisi za maafisa ustawi wa jamii kutoka halmashauri zote mbili za wilaya ya bunda katika kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya ya bunda kilichoketi  leo  7 Dec 2023.

Fausta Gabriel, afisa ustawi kutoka halmashauri ya wilaya ya Bunda

Akizungumzia hali ya ukatili wa kijinsia kwenye jamii afisa ustawi kutoka halmashauri ya mji wa bunda bi frolence gibogo amesema asilimia sitini ya kesi zinanopelekwa mahakamani zinazohusu ukatili zinatolewa hukumu huku asilimia 40 zikishindwa kutokana na baadhi ya watuhumiwa na wahanga kuharibu ushahidi au kukataa kutoa ushirikiano

Aidha amewataka wanajamii kwa ujumla kujitokeza kutoa taarifa za vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye jamii kwenye vyombo  husika  kama vile dawati la jinsia au ofisi za ustawi ngazi za halmashauri.