Mazingira FM

RC Mtambi aagiza fedha za ofisi za mitaa zitengwe kwa mujibu wa sheria

22 June 2026, 8:50 pm

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evance Alfred Mtambi

Amesema anatarajia kupokea taarifa ya utekelezaji wa maelekezo hayo katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha ifikapo mwezi Oktoba.

Na Adelinus Banenwa

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evance Alfred Mtambi, ameielekeza Halmashauri ya Mji wa Bunda kutenga fedha kwa ajili ya ofisi za serikali za mitaa kwa mujibu wa sheria, ambayo inaelekeza kutengwa kwa angalau shilingi 200,000 kwa kila robo ya mwaka.

Kanali Mtambi amesema anatarajia kupokea taarifa ya utekelezaji wa maelekezo hayo katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha ifikapo mwezi Oktoba.

Maelekezo hayo ameyatoa leo wakati wa kikao maalumu cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Bunda kilichoketi kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2024/2025, ambapo halmashauri hiyo ilipata hati inayoridhisha.

Baadhi ya madiwani Bunda TC kwenye baraza la madiwa la kupitia hoja za mkaguzi wa hesabu za serikali CAG
Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evance Alfred Mtambi

Mbali na hilo, Kanali Mtambi amezielekeza kamati zote za mitaa kufanya kazi kwa ufanisi zaidi, hususan Kamati za Afya na Mazingira, ili kuhakikisha usafi wa mazingira ndani ya Mji wa Bunda unasimamiwa ipasavyo.

Amesema hali ya usafi iliyopo kwa sasa hairidhishi kutokana na taka kuonekana katika maeneo mbalimbali ya mji huo, na kusisitiza kuwa viongozi na kamati husika wachukue hatua za haraka kurejesha mazingira safi na salama kwa wananchi.

mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Bunda Minza Shani
Sauti ya Kanali Evance Alfred Mtambi, Mkuu wa Mkoa wa Mara