Mazingira FM

Mamba waendelea kuleta maafa Buzimbwe

23 January 2024, 8:43 am

Mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina la Kulwa Mafwimbo 46 mkazi wa kijiji cha Buzimbwe ameshambuliwa na mamba wakati akioga ziwa Victoria.

Na Adelinus Banenwa

Mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina la Kulwa Mafwimbo 46 mkazi wa kitongoji cha Majengo kijiji cha Buzimbwe kata ya Butimba halmashauri ya wilaya ya Bunda mkoani Mara ameshambuliwa na mamba wakati akiendelea na shughuli za uvuvi ziwa Victoria.

Afisa tarafa ya Kekobyo Boniphas Maiga ameiambia Mazingira Fm kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa nane usiku hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa viongonzi wa kijiji, ambapo inatajwa Kulwa mbali na shughuli za uvuvi pia alikuwa anaoga.

Jitihada za kumtafuta Kulwa bado zinaendelea.

Viongozi wa serikali ya Kijiji tayari wamechukua hatua ikiwa ni pamoja na kuitisha wananchi Kwa ajili ya kuanza kumtafuta Mafwimbo lakini pia wameshatoa taarifa Kwa Maliasili ambao wamefika kutoa msaada.

Kwa njia ya Fm. 91.7
Website. Radiotadio.co.tz/mazingifm