Mazingira FM

Diwani wa kata ya Kisorya Bunda afariki dunia

15 March 2024, 12:59 pm

Diwani wa kata ya Kisorya enzi za uhai wake

Diwani wa kata ya Kisorya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda [CCM] Mhe Amos Lufunjo Ndaro amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo,

Na Adelinus Banenwa

Diwani wa kata ya Kisorya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda [CCM] Mhe Amos Lufunjo Ndaro amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo,

taarifa za awali kama zilivyothibitishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda mhe Charles Magafu Manumbu zinasema diwani huyo alikuwa haumwi

” sikuwa na taarifa ya yeye kuumwa na jana March 14, majira ya saa tano niliongea naye kwa simu tuliongea kuhusu jambo nikamwambia aende kwa mkurugenzi,

Nashangaa alfajiri ya saa kumi na moja kasoro dakika 20 leo March 15, 2024 napokea simu kwamba mhe diwani amefariki ”.

endelea kuifuatilia Mazingira fm kwa taarifa zaidi.