Mazingira FM

mashindano ya Quran Bunda Ally Hashimu Hakimu aibuka mshindi

21 April 2022, 5:37 pm

 

Ally Hashimu Hakimu ameibuka mshindi kwenye mashindano ya kutunza Quran tukufu wilaya ya Bunda

mashindano hayop yamefanyika leo April  16, 2022 katika msikiti wa Ijumaa Bunda mjini ambayo yameandaliwa na Kamati ya Kukuza na Kueneza Uislamu  Bunda huku mgeni rasmi akiwa ni Katibu tawala wilaya ya Bunda Salumu Halfani Mtelela

akizungumza na Mazingira Fm Ally Hashimu ambaye ni mshindi wa kwanza amesema kufuata maelekezo ya  mwalimu wake ndiyo siri pekee ya ushindi japo mashindano yalikuwa magumu

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya  mashindano hayondugu Said Jumanne Kizigo amesema pamoja na kuwa na muda mfupi wa maandalizi lakini washiriki wamejitokeza na malengo yameweza kutimia

Naye Salum Mtelela Katibu tawala wilaya ya Bunda ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mashinda hayo amezitaka kamati za kidini si tu kufundisha elimu za kiroho bali pia washiriki katika huduma nyingine za kijamii kama vile elimu na afya