Mazingira FM

WWF kuboresha chazo cha maji kisima cha Ryawaka- Rorya

28 September 2023, 3:14 pm

Wataalamu wa WWF pamoja na baadhi ya wakazi wa Rorya wakiwa katika chanzo cha maji.Picha na Thomas Masalu

Watalaamu wa Shirika la WWF leo 28 Sept 2023 wametembelea chanzo cha maji ya kisima cha Ryawaka kilichopo Kijiji cha Kwibuse Kata ya Kisumwa wilaya ya Rorya Mkoani Mara.

Na Thomas Masalu

Watalaamu wa Shirika la WWF leo 28 Sept 2023 wametembelea chanzo cha maji ya kisima cha Ryawaka kilichopo Kijiji cha Kwibuse Kata ya Kisumwa wilaya ya Rorya kwa lengo la kuangalia maendeleo ya chanzo hicho pamoja na utunzaji wa Mazingira katika eneo la kisima.

Wakazi wakiteka Maji kwenye kisima cha maji

Chanzo hicho cha maji kimefadhiliwa na WWF kwa kujengewe uzio pamoja na miti inayozunguka chanzo hicho ikiwa ni sehemu ya jitihada za kutunza Mazingira na vyanzo vya maji kwajili ya jamii inayozunguka chanzo hicho.

Kwa mujibu wa watalaamu wa Shirika la WWF, kisima hicho kinakusudiwa kuboreshwa zaidi kwa kujenga uzio mkubwa, kurudisha uoto wa asili kwa kupanda miti ya asili na kuwa chanzo cha kisasa.

Kisima hicho kimekuwa msaada mkubwa kwa wananchi hasa kipindi cha kiangazi ambapo hutumiwa na vijiji vitatu.