Mazingira FM

Bunda: watoto 3 wanusurika kifo nyumba ikiteketa kwa moto

26 August 2023, 9:19 pm

Baadhi ya mali zilizoungua ndani ya nyumba, Picha na Adelinus Banenwa

Watoto 3 wanusurika kifo nyumba ikiteketea kwa moto maeneo ya mtaa wa majengo kata ya kabarimu halmashauri ya mji wa Bunda mkoani mara huku chanzo kikitajwa ni mtoto kuchezea kiberiti.

Na Adelinus Banenwa

Watoto 3 wanusurika kifo nyumba ikiteketea kwa moto maeneo ya mtaa wa Majengo kata ya Kabarimu Halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara huku chanzo kikitajwa ni mtoto kuchezea kiberiti.

Wanafamilia wameiambia Mazingira Fm kuwa ulianza kuonekana moshi kabla ya moto kuonekana ukiteketeza vitu ambapo watoto hao walikuwa ndani wakiangalia luninga huku mtoto mmoja wapo akiwa anachezea kiberiti ambapo inatajwa alikuwa anawasha njiti na kuzizima.

Aidha wamesema kilichopelekea vitu kuteketea ni pamoja na mbanano wa makochi aina ya sofa ndani pamoja na magodoro yaliyokuwa dalini yamepelekea moto kushika na kuasambaa kwa haraka.

Baadhi ya mali zilizoungua ndani ya nyumba, Picha na Adelinus Banenwa
Wanafamilia
Baadhi ya mali zilizoungua ndani ya nyumba, Picha na Adelinus Banenwa

Naye mwenyekiti wa mtaa wa Majengo Mawazo Mussa amesema tukio hilo la moto ameliona akiwa kwenye msiba jirani na eneo hilo baada ya kuona moshi ukiwa umetanda juu na sauti za kuomba msaada ambapo alichukua jukumu la kufika moshi ulipokuwa ukitoka na kukuta nyumba ikiungua.

mwenyekiti wa mtaa wa majengo Mawazo musa

Aidha ameiomba serikali kupeleka huduma ya vikosi vya zimamoto na uokoaji kila wilaya ili huduma iwepo karibu na wananchi ili wanapopata tatizo waweze kupata msaada kwa haraka.

mwenyekiti wa mtaa wa majengo Mawazo musa