Mazingira FM

CCM Bunda yakanusha kubeba watu kwenye mikutano

15 May 2026, 8:53 pm

Katibu wa siasa uenezi na mafunzo wilaya ya Bunda ndugu Gasper Petro Charles

Gasper amesema chama hicho kina utaratibu wake na wakati wa ziara za viongozi huundwa kamati mbalimbali ambazo huratibu mikutano ambapo moja ya kamati hizo huwa ni ya usafiri.

Na Adelinus Banenwa

Chama cha mapinduzi wilaya ya bunda kimekanusha uvumi ambao husemwa na watu kuwa huwa wanasomba watu hasa wanachama pindi ziara za viongozi zinapofanyika katika wilaya hiyo.

Katibu wa siasa uenezi na mafunzo wilaya ya Bunda ndugu Gasper Petro Charles amekanusha kauli hiyo wakati akizungumza kupitia kipindi cha duru za Habari kinachorushwa na radio mazingira fm ambapo amesema mara kadhaa watu wamekuwa wakisema chama hicho husomba watu wakati wa mikutano au nziara za viongozi wa kitaifa wanapokuja Bunda kauli ambayo amesema ni upotoshaji.

Gasper amesema chama hicho kina utaratibu wake na wakati wa ziara za viongozi huundwa kamati mbalimbali ambazo huratibu mikutano ambapo moja ya kamati hizo huwa niya usafiri hivyo kupitia kamati hiyo uhakikisha wanachama wanafika eneo la mkutano kwa namna yoyote bila usumbufu hasa ukizingatia eneo la kijiografia la wilaya ya Bunda na utaratibu huo ufanyika katika ziara au mikutano ya chama inayofanyika kiwilaya siyo kimajimbo.

Gasper ameeleza hayo akijibu swali la mtangazaji kuhusu utaratibu wa chama kuwafikisha wanachama eneo la mkutano katika ziara ya katibu wa NEC siasa na uenezi Ndugu Kenani Kihongosi aliyeko mkoani Mara kwa ziara ya chama huku akitarajiwa kufika na kufanya mkutano wa hadhara wilayani hapa siku ya jumapili  May 17 2026 katika viwanja vya CCM wilaya ya Bunda.

Katibu wa siasa uenezi na mafunzo wilaya ya Bunda ndugu Gasper Petro Charles