Mazingira FM

Kulwa Kahabi : Nitatoa milioni 17 ujenzi jiko la kupikia

19 October 2023, 8:42 pm

Mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM taifa Kulwa Kahabi. Picha na Godfrey Christopher

Zaidi ya shilingi milioni kumi na saba  zimeahidiwa  kutolewa na mdau wa maendeleo ambae pia ni mjumbe wa mkutano mkuu wa ccm taifa Kulwa Kahabi ili kusaidia ujenzi wa jiko la  kupikia chakula cha wanafunzi  katika shule ya sekondari Sazira iliyopo kata ya Sazira wilaya ya Bunda.

Mussa Kagole na Godfrey Christopher

Zaidi ya shilingi milioni kumi na saba  zimeahidiwa  kutolewa na mdau wa maendeleo ambae pia ni mjumbe wa mkutano mkuu wa ccm taifa Kulwa Kahabi ili kusaidia ujenzi wa jiko la  kupikia chakula cha wanafunzi  katika shule ya sekondari Sazira iliyopo kata ya Sazira wilaya ya Bunda

Akizungumza katika mahafali ya 16 ya kidato cha nne shuleni hapo ambapo ndiye aliekuwa mgeni rasmi amesema ametoa fedha hizo ili zitumike kujenga nyumba hiyo ya kupikia chakula cha wanafunzi, ili wapishi waepukane na changamoto za hali ya hewa ,kama vile mvua na upepo ambazo ndio zimekua changamoto kubwa kwa shule hiyo

Sauti ya Kulwa Kahabi
Mkuu wa shule ya Sekondari Sazira Ndg Edigar Sibola. Picha na Godfrey Christopher

Aidha Ndug  Kahabi amewataka wahitimu wote wa kidato cha nne shuleni hapo kutojihusisha na makundi mabaya mtaani na kuwasihi waendelee kujilinda na changamto zozote zitakazo wakuta mtaani mara baada ya kuhitimu masomo yao ya kidato cha nne wakiwa wanasubili matokeo

Sauti ya Kulwa Kahabi
Wanafunzi kidato cha nne Sekondari Sazira. Picha na Godfrey Christopher
Wanafunzi kidato cha nne Sekondari Sazira. Picha na Godfrey Christopher

Awali wakisoma risala wanafunzi wa kidato cha nne wamesema changamoto kubwa shuleni hapo ni jiko la kupikia chakula cha wanafunzi  jambo linalosababisha changamoto katika uandaaji wa chakula hasa kipindi cha mvua.

sauti ya wahitimu