Mazingira FM

Katibu mkuu BAVICHA alia na wazee

21 April 2024, 1:05 pm

Yohana Kaunya, katibu mkuu BAVICHA Tanzania Bara akiwa katika studio za Radio Mazingira Fm, Picha na Edward Lucas

Changamoto kubwa inayowafanya vijana washindwe kuwania nafasi za uongozi ” ni wazee kutowaamini vijana, vijana wengi hawaaminiwi na wazee”

Na Edward Lucas

Katibu mkuu wa Baraza la Vijana Chadema Tanzania Bara, Yohana Kaunya amesema wazee kutowaamini vijana na ushirikishwaji mdogo wa vijana ni miongoni mwa changamoto zinazokwamisha juhudi za vijana kuwania nafasi za uongozi katika jamii.

Kaunya amesema hayo leo akiwa mgeni katika kipindi cha Siasa na Maendeleo studio za Radio Mazingira Fm kuzungumzia ushiriki wa vijana katika kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kuelekea uchaguzi ujao Tanzania.

Amesema “vijana walio wengi hawaaminiwi na wazee kwamba tukimruhusu kwenda kugombea huyu inakuwa ni changamoto kushinda lakini kumbe kuna mtu anauwezo wa kushinda”

Aidha ameongeza kuwa ushirikishwaji mdogo, sheria za uchaguzi, michakato ya ndani ya vyama ni miongoni mwa mambo ambayo yamekuwa yakiwakatisha tamaa vijana kushiriki katika uchaguzi

Sauti ya Yohana Kaunya, katibu mkuu BAVICHA Bara