Mazingira FM

Majanga ya mvua Mara, watatu wapoteza maisha maeneo tofauti

5 December 2023, 8:19 am

Watatu wapoteza maisha kwa kusombwa na maji maeneo tofauti mkoani Mara

Na Adelinus Banenwa

Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Maduhu Isinde Ikerege mkazi wa mtaa wa Changuge kata ya Mcharo Bunda mjini anatajwa kupoteza maisha kwa kusombwa na maji wakati akitafuta mifugo yake iliyopotea.

Akizungumza na Mazingira FM Bunuri Mgendi ambaye ni mke wa Maduhu anasema mume wake aliondoka asubuhi ya tarehe 3 Disemba kwenda maeneo ya mto Rubana kutafuta ng’ombe wake wawili waliopotea siku ya jana yake.

Aidha Bunuri ameendelea kusema kuwa majira ya saa tano asubuhi ndipo alipata taarifa za mume wake kusombwa na maji wakati akijaribu kuvuka mto rubana kwenda ng’ambo kutafuta mifugo yake hiyo iliyopotea.

Bunuri amesema amezaa na Maduhu watoto 10

Naye mwenyekiti wa mtaa wa Changuge Kinyunyi Chamtigiti amethibitishi kuwepo Kwa tukio hilo ambapo amesema tukio hilo amepokea taarifa tangu saa tatu asubuhi ambapo aliitiaha kikao Cha yowe Kisha walianza zoezi la utafutaji lilianza ambapo hadi sasa zoezi linaendele la kumtafuta mkazi uyo .

Mwenyekiti Kinyunyi amesema Kwa Sasa changamoto kubwa ni kuongezeka Kwa maji ya mto rubana bia uchache wa timu ya uogeleaji.

mwenyekiti wa mtaa wa Changuge Kinyunyi Chamtigiti

Emmanuel Kija Katibu wa mbunge wa Bunda mjini Robert Maboto amefika kwenye familia hiyo na kutoa Salam za pole kwao huku akiwataka wazazi na walezi kuchuku tahadhari hasa kipindi hiki Cha mvua zinazoendelea .

Emmanuel Kija Katibu wa mbunge wa Bunda mjini

kwingineko

Watoto wawili wakazi kitongoji cha mbugani, Kijiji Cha mwibagi, kata ya Kyanyari wilaya ya Butiama wamepoteza maisha Kwa kusombwa na Maji.

Akizungumza na Mazingira Fm Mwenyekiti wa kitongoji Cha Mbugani Malongo Kusekwa Mnata amesema tukio hilo limetokea asubuhi ya tarehe 3 mwezi dec ambapo watoto hao wakiwa wanachunga mifugo waliamua kuingia kwenye mkondo wa maji ili waogelee lakini maji yaliwazidi nguvu na kuwasomba

Kusekwa amesema mkondo huo wa maji mara nyingi hujaa maji kipindi Cha Mvua ambapo mkondo huo wa maji yanamwaga maji yake kwenye mto Suguti.

Mwenyekiti wa kitongoji Cha Mbugani Malongo Kusekwa Mnata