Mazingira FM

DC Naano: Bunda inaongoza kwa kutokuwa na vyoo Mara

16 August 2023, 9:50 am

Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe. Dr,Vicent Naano

Bunda ni miongoni mwa wilaya zinaongoza kwa kutokuwa na vyoo mkoani Mara

Na Thomas Masalu

Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe. Dr,Vicent Naano amegiza kushughulikiwa kikamilifu suala la usafi wa mazingira hasa kuwa na vyoo bora majumbani ili kusaidia kupunguza magonjwa yatokanayo na uchafu wa mazingira.
Dr, Naano ametoa agizo hilo leo katika mkutano wa wadau wa kilimo ambapo amesema wilaya ya Bunda ni miongoni mwa wilaya zinaongoza kwa kutokuwa na vyoo hali hiyo kupelekea kukosa fukwe, hoteli na wawekezaji kutokana na kuzaga kwa vinyesi.

Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe. Dr,Vicent Naano

Katika hatua nyingine mkuu huyo ameagiza wenyeviti wa vitongoji, vijiji na kata kuhamasisha wananchi kuhudhuria mikutano inayoandaliwa kujadili changamoto zinazowakabili.

Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe. Dr,Vicent Naano