Mazingira FM

DC Naano apongeza usimamizi wa miradi Bunda

9 December 2023, 3:49 pm

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dr Vicent Aney Naano, Picha na Adelinus Banenwa

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dr Vicent Aney Naano ameipongeza halamashauri ya wilaya ya Bunda kwa usimamizi mzuri wa miradi inayotekelezwa.

Na Adelinus Banenwa

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dr Vicent Aney Naano ameipongeza halamashauri ya wilaya ya Bunda kwa usimamizi mzuri wa miradi inayotekelezwa katika pindi cha hivi karibuni Dr Naano ameyasema hayo wakati akihutubia kikao cha robo ya kwanza cha baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Bunda kilichoketi 8 Dec 2023.

Mkuu huyo wa wilaya amesema tangu asisiteze suala la usimamizi mzuri wa miradi halmashauri ya wilaya ya Bunda imesimamia vizuri miradi yake kama vile mradi wa nyumba za walimu shule za sekondari za Tirina kutoka jimbo la Bunda na Sunsi kutoka jimbo la mwibara.

Sauti ya mkuu wa wilaya

Aidha DC naano ameielekeza halmashauri kutunga sheria ndogo ya kuwawajibisha wananchi wanaokataa kuudhuria mikutano ya viongozi inayoitishwa katika maeneo yao.

Sauti ya mkuu wa wilaya
Picha na Adelinus Banenwa
Picha na Adelinus Banenwa