Mazingira FM

Baraza la madiwani Bunda laahirishwa madiwani wakidai taarifa za miradi

16 November 2023, 9:49 pm

Changwa Mkwazu, Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Bunda katika mkutano wa Baraza akifafanua baadhi ya hoja. picha na Edward Lucas

Madiwani wakataa kuendelea na kikao wakiomba kupata taarifa za miradi mbalimbali inayotekelezwa ndani ya halmashauri.

Na Edward Lucas.

Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Mkoani Mara, Mhe. Charles Manumbu ameahirisha kikao cha baraza hilo na kumwagiza Mkurugenzi kuandaa taarifa ya ukaguzi wa mradi wa kuhimili athari za Mabadiliko ya Tabianchi (BCRAP) unaotekelezwa katika halmashauri hiyo na kuiwasilisha Kamati ya Fedha.

Mhe. Charles Manumbu, Mwenyekiti Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Bunda akitoa maelekezo ya kuahirisha baraza.

Aidha Mhe. Manumbu amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri kuandaa mpango kwa wajumbe wote wa Kamati ya Mradi iliyokuwepo mwanzoni kukutana na Kamati ya Fedha ili kila mmoja ahojiwe kujua ni wapi alishiriki na alishiriki kwa namna gani.

Sauti ya Mhe. Manumbu akitangaza kuahirisha kikao

MANUMBUUamuzi huo wa Mwenyekiti umekuja kufuatia hoja za madiwani kuomba kuahirishwa kwa kikao hicho wakitaka kupokea taarifa za utekelezaji wa miradi mbalimbali mikubwa katika halmashauri hiyo ikiwemo mradi wa kuhimili athari za Mabadiliko ya Tabianchi (BCRAP) na Mradi wa Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Mkoa wa Mara.

Awali akitoa hoja ya kuahirishwa kwa kikao hicho, Diwani wa kata ya Mugeta, Muganga Jongora amesema, kwa changamoto wanazoziona kwa miradi ya Bunda analiomba baraza liahirishwe mpaka pale Kamati ya Fedha itakapopokea taarifa ya Ukaguzi wa mradi husika.

Mhe. Mganga Jongora
Madiwani wakichangia hoja ya kuahirisha kikao Cha Baraza.

Hoja hiyo iliungwa mkono na wajumbe walio wengi kabla ya Mwenyekiti wa kikao kuhitimisha hoja kwa kupigiwa kura ambapo wengi walipitisha kuahirisha kikao

Madiwani katika hoja ya kuahirisha kikao