Mazingira FM

Bunda yajipanga kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi

10 March 2022, 8:20 pm

watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda wakiwa kwenye mafunzo ya Mpango wa mabadiliko ya tabia ya nchi

Zaidi ya Bilion 3.4 zimetolewa kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Bunda katika utekelezaji wa Mpango wa mabadiliko ya tabia ya nchi

Akizungumza katika mafunzo maalumu ya usimamizi wa fedha za miradi yaliyofanyika Leo march 10, 2022 kwa Madiwani na wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Dr Masinde Bwire kutoka kamisheni ya Bonde la ziwa Victoria amesema mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wasimamizi wa mradi huo ili uweze kuleta ufanisi na tija kwa wananchi

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Wakiwa kwenye mafunzo ya Mpango wa mabadiliko ya tabia ya nchi

Kwa upande wake Fredrick Mulinda ambaye ni Afisa kutoka NEMC amesema mafunzo ya utawala bora kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda na Madiwani yanafanyika kwa lengo la kuhakikisha mradi kusudiwa unatekelezwa, kusimamiwa na kuwafikia walengwa kama ulivyopangwa, Na kwamba mafunzo hayo yatakuwa endelevu.

Naye Dickson Balige afisa mipango Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ambaye pia ni msimamizi wa mradi huu wa kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda amesema mradi huu utatekelezwa kwa miaka mitatu ambapo utazingatia katika nyanja kuu Nne ambazo ni kilimo, ufugaji, uvuvi na ufugaji wa nyuki huku akiwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa wataalamu wataofika kwenye maeneo yaliyoanishwa kwenye utekelezaji wa Mpango huu