Mazingira FM

Bobaboda wapewa onyo kali kujichukulia sheria mkononi

2 March 2024, 6:05 pm

Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi mhe Jumanne Sagini amekemea madereva pikipiki maarufu kama bodaboda kukiuka sheria za usalama barabarani.

Na Adelinus Banenwa

Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi mhe Jumanne Sagini amekemea madereva pikipiki maarufu kama bodaboda kukiuka sheria za usalama barabarani.

Mhe sagini amesema hayo katika kata ya Komuge wilayani Rorya katika ziara ya Mhe waziri mkuu Kasim Majaliwa ambapo amesema kutokana na tukio la Jana ambapo madereva bodaboda walichoma moto gari la abilia kampuni ya Saibaba baada ya kumgonga mwendesha bodaboda

Mhe sagini amesema tabia ya madereva bodaboda kukiuka sheria za usalama barabarani na kujichukulia Sheria mkononi

Pia Mhe Sagini amesema tabia zao ni kuingia kwenye barabara kuu kwa mwendo mkali jambo ambalo halikubariki