Mazingira FM
Mazingira FM
26 April 2026, 11:59 am

Lengo si tu serikali kupata ushuru bali inasaidia usalama wa abiria pamoja na kupunguza usumbufu kwao.
Na Adelinus Banenwa
Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Aswege Enock Kaminyoge amemuelekeza mkuu wa polisi Bunda na mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Bunda kuhakikisha magari yote ya abiria yanaingia stendi ya wilaya ya Bunda.
DC Aswege amesema hayo leo April 26, 2026 wakati akizungumza na wananchi eneo la stendi mpya wilayani Bunda wakati wa zoezi la usafi katika maadhimisho ya miaka 62 ya Muungano .
Amesema kama yalivyo maeneo mengine magari yote ya abiria ni lazima yapitie stendi ambapo lengo si tu serikali kupata ushuru bali inasaidia usalama wa abiria pamoja na kupunguza usumbufu kwao huku akitoa tahadhari kuwa maelekezo hayo hayakatazi abiria hao kushuka au kupanda kwenye vituo vya Nyasura na Bunda DDH.
Baadhi ya mawakala wa mabasi katika stendi hiyo wamepongeza maelekezo hayo ya mkuu wa wilaya huku wakisema wanasubiri utekelezaji.
Wamesema suala la mabasi kugoma kuingia stendi limepigiwa kelele muda mrefu lakini malalamiko hayo hayakufanyiwa kazi jambo linalosababisha usumbufu kwa abiria.
BBBBBBBBBBBBBBBBBBB