Mazingira FM

Mabotto kuwasomesha wanafunzi watakaofaulu kwa daraja la kwanza

19 October 2023, 9:17 pm

Katibu wa mbunge wa jimbo la Bunda mjini Emmanuel Kija, Picha na Edward Lucas

Mbunge Robert Maboto ameahidi kuwafadhili vifaa vya shule  wakati wa kujiunga na kidato cha Tano wanafunzi wote  shule ya Sekondari Wariku na Dr. Nchimbi watakaopata daraja la kwanza katika matokeo ya kidato cha nne kwenye  mtihani wa taifa unaotarajiwa kifanyika mwezi November  mwaka huu.

Na Adelinus Banenwa Na Edward Lucas

Mbunge Robert Maboto ameahidi kuwafadhili vifaa vya shule  wakati wa kujiunga na kidato cha Tano wanafunzi wote shule ya Sekondari Wariku na Dr. Nchimbi watakaopata daraja la kwanza katika matokeo ya kidato cha nne kwenye  mtihani wa taifa unaotarajiwa kifanyika mwezi November  mwaka huu.

Ahadi hiyo imetolewa na Emmanuel Kija katibua wa mbunge katika mahafali ya 16 kidato cha nne shule ya sekondari Wariku iliyopo kata ya Wariku wilayani Bunda ambapo alifika kumuwakilisha mgeni rasmi Mhe Mabotto.

Aidha katika hatua nyingine kiasi cha shilingi milioni moja na elfu kumi zimetolewa na mbunge huyo katika ukamilishaji wa ujenzi wa choo shule ya sekondari Wariku iliyopo halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara

Fedha hizo zimetolewa na katibu wa mbunge wa jimbo la Bunda mjini Emmanuel Kija katika mahafali hiyo ya kidato cha nne ya shule hiyo ambapo amesema Mhe mbunge kipaumbele chake katika jimbo ni suala la elimu ndo maana kupitia fedha za mfuko wa jimbo na hata fedha zake binafsi kwa kiasi kikubwa anazielekeza kwenye  sekta ya  elimu.

Sauti ya Emmanuel Shija Nkwama katibu wa mbunge
Bwire Mashauri mkuu wa shule ya sekondari wariku, Picha na Edward Lucas

Bwire Mashauri mkuu wa shule ya sekondari wariku amesema shule hiyo imepata mafanikio mengi hasa ya kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne wanaotarajia kuhitimu hivi karibuni ikiwemo mwanafunzi mmoja kupata daraja la kwanza ya alama nane katika mtihani wa halmashauri ya mji wa bunda

Aidha amesema pamoja na mafanikio hayo zipo changamoto mbalimbali zinazokabili shule hiyo ikiwemo ushirikiano duni kutoka kwa wazazi, wazazi kutofuatilia maendeleo ya watoto wao utoro wa wanafunzi unaosababishwa na wazazi miongoni mwa changamoto zingine.

Sauti ya Bwire Mashauri

Awali wakisoma risala mbele ya mgeni rasmi wanafunzi wahitimu wamesema walianza kidato cha kwanza wakiwa jumla ya wanafunzi  140  lakini kutokanana na changamoto mbalimbali wanahitimu wanafunzi  87 wavulana 43   na wasichana 44.

Aidha wamesema kuna baadhi ya chanagamoto za ukosefu wa maji safi na salama shuleni hapo, upungufu wa walimu hasa wa masomo ya sayansi upungufu wa matundu ya vyoo miongoni mwa changamoto zingine.

Sauti ya wahitimu